Russia yamuunga mkono kamanda wa jeshi la Libya
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Russia na Kamanda wa jeshi la taifa la Libya wamefanya mazungumzo kuhusu kuendeleza ushirikiano wa kijeshi kati ya pande mbili.
Wizara ya Mambo ya Nje ya Russia imeripoti kuwa, Michail Bogdanov Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Russia amesisitiza katika mazungumzo yake na Khalifa Haftar, kamanda wa jeshi la taifa la Libya huko Moscow kuhusu msimamo wa Russia katika kuunga mkono mchakato wa kisiasa nchini Libya.
Viongozi hao wa Libya na Russia wamebadilishana mawazo kuhusu matukio ya Libya na wakasisitiza kuhusu umuhimu wa kufanyika mazungumzo mapana kwa kuyashirikisha makundi yote ya kisiasa na uongozi wa maeneo mbalimbali ili kuiondoa Libya katika mgogoro wa kisiasa unaoikabili.
Bogdanov ameunga mkono kulindwa umoja wa wananchi na wa ardhi nzima ya Libya. Wakati huo huo duru za Marekani na Misri zimearifu kuwa kikosi maalumu cha wanajeshi kimetumwa katika kambi za kijeshi huko Misri karibu na mpaka na Libya.