Uchumi wa nchi za kusini mwa Sahara waitia wasi wasi Côte d’Ivoire
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i27360-uchumi_wa_nchi_za_kusini_mwa_sahara_waitia_wasi_wasi_côte_d’ivoire
Serikali ya Côte d’Ivoire imeoyesha wasi wasi juu ya mwendelezo wa kushuka kiwango cha uchumi wa nchi za kusini mwa Sahara, barani Afrika.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Apr 06, 2017 03:07 UTC
  • Uchumi wa nchi za kusini mwa Sahara waitia wasi wasi Côte d’Ivoire

Serikali ya Côte d’Ivoire imeoyesha wasi wasi juu ya mwendelezo wa kushuka kiwango cha uchumi wa nchi za kusini mwa Sahara, barani Afrika.

Hayo yamesemwa na Daniel Kablan Duncan, Makamu wa Rais wa Côte d’Ivoire katika kikao cha kimataifa cha siku moja kilichopewa anwani ya 'Kupatikana Mustakbali Tegemezi wa Afrika' ambacho kilifanyika mjini Abidjan, ambapo alisema kuwa, mwaka uliopita, kiwango cha uchumi wa nchi za kusini mwa sahara kilipungua sana.

Daniel Kablan Duncan, Makamu wa Rais wa Côte d’Ivoire

Kwa mujibu wa Kablan Duncan, mporomoko wa kiwango hicho haujawahi kushuhudiwa kwa kipindi cha miaka sita iliyopita. Hii ni katika hali ambayo ongezeko la uchumi la asilimia tano, kiliripotiwa mwaka 2011 katika nchi za eneo hilo. Kadhalika makamu wa rais wa Côte d’Ivoire amesema kuwa kwa mara ya kwanza na katika kipindi cha miaka 10, nchi za Afrika zimekumbwa na changamoto mbalimbali kukiwemo kupungua malighafi uwekezaji wa moja kwa moja wa kigeni kutokana na matatizo ya mabadiliko ya hali ya hewa ambako kumeenda sambamba na taathira mbaya kwa uchumi.

Hali ya mporomoko wa Uchumi 

Kikao hicho cha kimataifa kimehudhuriwa na wawakilishi wa nchi za Kiafrika, Benki ya Uwekezaji ya Ulaya BEI, Benki ya Ustawi ya Afrika BAD na Benki ya Magharibi mwa Afrika BOAD.