Watu 22 wameuawa katika machafuko baada ya uchaguzi Uganda
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i3043-watu_22_wameuawa_katika_machafuko_baada_ya_uchaguzi_uganda
Polisi ya Uganda imetangaza kuwa mapigano yaliyojiri magharibi mwa nchi hiyo kati ya wafuasi wa wagombea uchaguzi wanaohasimiana ambao walishiriki katika uchaguzi mkuu wa nchi hiyo yameuwa watu 22 na kuwajeruhi wengine 10.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Mar 14, 2016 12:49 UTC
  • Watu  22 wameuawa katika machafuko baada ya uchaguzi Uganda

Polisi ya Uganda imetangaza kuwa mapigano yaliyojiri magharibi mwa nchi hiyo kati ya wafuasi wa wagombea uchaguzi wanaohasimiana ambao walishiriki katika uchaguzi mkuu wa nchi hiyo yameuwa watu 22 na kuwajeruhi wengine 10.

Chama cha upinzani cha Mabadiliko ya Demokrasia (FDC) kimeituhumu serikali ya Uganda kuwa imechochea machafuko hivi karibuni katika eneo ambalo mgombea wa upande wa upinzani Kizza Besigye ana uungaji mkono mkubwa dhidi ya kiongozi mkongwe Yoweri Museveni ambaye alishinda uchaguzi wa rais uliofanyika nchini humo tarehe 12 Februari huku ukigubikwa na udanganyifu.

Polisi ya Uganda ilisema katika taarifa iliyotoa jana kuwa ghasia ziliibuka kati ya wafuasi wa wagombea hasimu baada ya kufanyika uchaguzi wa serikali za mitaa katika eneo hilo tarehe 24 Februari. Polisi imesema kuwa raia 16 waliaga dunia kwenye machafuko wakati wafuasi wa wagombea hao wanaohasimiana, na wengine 6 waliaga dunia baada ya polisi kuingilia kati ili kuzima ghasia hizo. Mbali na kuuawa watu hao, watu wengine 10 walijeruhiwa wakiwemo wanajeshi wanne, huku nyumba 149 zikichomwa moto.