Gazeti la Quds al-Arabi: Mgogoro wa Morocco hautatatuliwa kijeshi
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i31030-gazeti_la_quds_al_arabi_mgogoro_wa_morocco_hautatatuliwa_kijeshi
Mtandao wa habari wa gazeti la Quds al-Arabi limeandika kuwa, mgogoro wa malalamiko ya raia wa eneo la kaskazini mwa Morocco, hauwezi kutatuliwa kwa kutumia mabavu, bali utatatuliwa kwa kutekeleza malalamiko ya wananchi.
(last modified 2025-11-15T07:02:39+00:00 )
Jun 27, 2017 15:07 UTC
  • Gazeti la Quds al-Arabi: Mgogoro wa Morocco hautatatuliwa kijeshi

Mtandao wa habari wa gazeti la Quds al-Arabi limeandika kuwa, mgogoro wa malalamiko ya raia wa eneo la kaskazini mwa Morocco, hauwezi kutatuliwa kwa kutumia mabavu, bali utatatuliwa kwa kutekeleza malalamiko ya wananchi.

Mtandao wa gazeti hilo umeandika hayo Jumanne ya leo kwamba, wakazi wa eneo la kaskazini mwa Morocco ukiwemo mji wa Al Hoceima walipewa ahadi nyingi na viongozi wa nchi hiyo kwa ajili ya kutatua matatizo yao, hivyo maandamano hayo ni njia pekee ya kuwashinikiza viongozi hao wa serikali kutekeleza matakwa yao.

Maandamano yakiendelea

Sambamba na kuashiria kuwa, baadhi ya viongozi wa serikali ya Rabat wanakusudia kutumia nguvu kubwa kwa ajili ya kukandamiza maandamano hayo, limeandika kwa kusema, viongozi hao wanaamini kuwa kuendelea malalamiko ya wakazi hao wa kaskazini mwa nchi hiyo, kunatia dosari itibari na nafasi ya serikali na kwamba ikiwa maandamano hayo hayatazimwa haraka, basi nchi hiyo haitokuwa na uwezo wa kuzima tena malalamiko na maandamano hapo baadaye.

Hii ni katika hali ambayo maandamano hayo yameingia mwezi wa nane sasa. Inafaa kuashiria kuwa, serikali ya Morocco yenye vyama tofauti vya siasa na vituo mbalimbali vya sheria, haijaweza kuupatia ufumbuzi mgogogro unaonedelea nchini kutokana na kujikita katika upatanishi wa migogoro ya kimataifa kama vile, Libya, Qatar na nchi nyingine za Kiafrika.

Mouchine Fikr aliyeuawa aliyeuawa kikatili na polisi ya Morocco

Maandamano ya hivi karibuni yaliibuka kufuatia mauaji dhidi ya muuza samaki anayejulikana kwa jina la Mouchine Fikr aliyeuawa na polisi wa serikali katika mji wa Al Hoceima. Muuza samaki huyo aliuawa kwa kufinywafinywa na mashine ya gari la kuzoa taka wakati akijaribu kuchukua samaki wake aliokuwa akiwauza ambao walichukuliwa na polisi na kutupwa katika gari hilo la kuzoa taka.