Mfalme wa Morocco asisitiza kushiriki vyema nchi hiyo katika AU
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i33448-mfalme_wa_morocco_asisitiza_kushiriki_vyema_nchi_hiyo_katika_au
Mfalme Mohamed wa Sita wa Morocco amesema kuwa, kujiunga tena nchi hiyo katika Umoja wa Afrika (AU) ni hatua muhimu na yenye taathira.
(last modified 2026-02-21T22:51:18+00:00 )
Aug 21, 2017 11:18 UTC
  • Mfalme wa Morocco asisitiza kushiriki vyema  nchi hiyo katika AU

Mfalme Mohamed wa Sita wa Morocco amesema kuwa, kujiunga tena nchi hiyo katika Umoja wa Afrika (AU) ni hatua muhimu na yenye taathira.

Mfalme Mohammed wa Sita wa Morocco ameashiria uhusiano ulioko kati ya nchi hiyo na nchi nyingine za bara la Afrika na kusisitiza kuwa kuwepo Morocco katika Umoja wa Afrika ni jambo lenye umuhimu na kwamba serikali ya Rabat inalipa kipaumbele kikubwa suala la kuwepo nchi hiyo ndani ya AU kwa ajili ya kudhamini maslahi ya pamoja. 

Mfalme wa Morocco amesema, kuwepo nchi yake katika Umoja wa Afrika kunakumbushia hisia za uaminifu wa kihistoria ya pamoja wa pande na kwamba, hamu na kubeba majukumu kwa serikali na wananchi wa Morocco kwa bara la Afrika kunaashiria irada thabiti na mustakbali wa pamoja wa pande hizo. 

Umoja wa Afrika (AU) uliafiki rasmi kujiunga tena Morocco na jumuiya hiyo katika mkutano wa 28 wa umoja huo uliofanyika mwezi Januari mwaka huu baada ya kupita miongo mitatu. Morocco ilijiondoa katika Umoja wa Nchi Huru za Kiafrika mwaka 1976.