Ikwani: Hatutatambua rasmi chaguzi zote za Misri
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i34583-ikwani_hatutatambua_rasmi_chaguzi_zote_za_misri
Harakati ya Ikhwanul Muslimin ya Misri imetangaza kuwa haitatambua rasmi uchaguzi wowote ule utakaofanyika nchini humo.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Sep 19, 2017 23:23 UTC
  • Ikwani: Hatutatambua rasmi chaguzi zote za Misri

Harakati ya Ikhwanul Muslimin ya Misri imetangaza kuwa haitatambua rasmi uchaguzi wowote ule utakaofanyika nchini humo.

Gazeti la al Quds al Arabi limeripoti kuwa, msemaji wa harakati ya Ikhwanul Muslimin ya Misri, Tal'at Fahmi amesema, uchaguzi wowote ule utaofanyika Misri ukiwemo wa Rais, Bunge na serikili za mitaa utakuwa batili kwa mujibu wa katiba iwapo hautamshirikisha rais aliyeondolewa madarakani wa nchi hiyo, Muhammad Morsi.

Fahmi ameongeza kuwa, Morsi ndiye rais halali wa Misri na hakukabidhi madaraka yake kwa mtu mwingine. 

Muhammad Morsi anashikiliwa katika jela ya Misri

Hii ni mara ya kwanza kwa harakati ya Ikhwanul Muslimin kutangaza msimamo wake kuhusu uchaguzi wa rais uliopangwa kufanyika mwakani nchini Misri. 

Jenerali Abdul Fattah al Sisi akitwaa madaraka ya Misri mwaka 2013 kupitia mapinduzi ya kijeshi yaliyomuondoa madarakani Muhammad Morsi. Baada ya kutwaa madaraka, al Sisi alipiga marufuku shughuli zote za harakati ya Ikhwanul Muslimin na kuwatia nguvuni viongozi na wanachama wengi wa harakati hiyo kubwa zaidi ya kisiasa nchini Misri.