Askari wa serikali ya Kongo DR watuhumiwa kuhusika na mauaji ya raia
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i34757-askari_wa_serikali_ya_kongo_dr_watuhumiwa_kuhusika_na_mauaji_ya_raia
Wakimbizi katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wamewatuhumu maafisa usalama wa serikali kuwa wamehusika katika mauaji ya raia.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Sep 24, 2017 00:01 UTC
  • Askari wa serikali ya Kongo DR watuhumiwa kuhusika na mauaji ya raia

Wakimbizi katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wamewatuhumu maafisa usalama wa serikali kuwa wamehusika katika mauaji ya raia.

Kamishna Mkuu wa Wakimbizi ya Umoja wa Mataif (UNHCR) nchini Zambia, Prine Ilarra, imewanukuu wakimbizi hao wakisema kuwa, maafisa usalama wa Kongo DR, wanawakihusika na mauaji ya raia katika maeneo yenye mapigano na waasi. Ilarra ameongeza kuwa,  machafuko yanayoendelea katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo yamewafanya zaidi ya raia elfu sita wa nchi hiyo kukimbilia Zambia na kwamba, serikali ya Lusaka imepatwa na wasiwasi kutokana na uwezekano wa kuibuka mgogoro wa kibinadamu. 

Wanamgambo wanaopigana na serikali katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo

Kamishna Mkuu wa Wakimbizi ya Umoja wa Mataif nchini Zambia amesema kuwa,  maafisa usalama wa serikali ya Kinshasa wametajwa kuhusika katika kuchoma moto makazi ya raia, kubakaji na kupora mali za raia.

Hadi sasa maelfu ya raia wa taifa hilo wamekuwa wakimbizi kutokana na mapigano kati ya waasi na askari wa serikali hususan katika maeneo ya mashariki na kaskazini mwa taifa hilo la katikati mwa Afrika.