Waislamu Tanzania washiriki kwenye maombolezo ya Imam Hussein AS
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i34897-waislamu_tanzania_washiriki_kwenye_maombolezo_ya_imam_hussein_as
Waislamu wanajumuika katika Msikiti wa Al Ghadir mjini Dar es Salaam nchini Tanzania kwa ajili ya maombolezo ya kuuawa shahidi Imam Hussein AS katika mwezi wa Muharram.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Sep 27, 2017 00:48 UTC
  • Waislamu Tanzania washiriki kwenye maombolezo ya Imam Hussein AS

Waislamu wanajumuika katika Msikiti wa Al Ghadir mjini Dar es Salaam nchini Tanzania kwa ajili ya maombolezo ya kuuawa shahidi Imam Hussein AS katika mwezi wa Muharram.

Kwa mujibu wa Shirika  Shirika la Habari za Qur'ani la Kimataifa (IQNA), Waislamu wa matabka mbali mbali, aghalabu wakiwa Waislamu wa madhehebu ya Shia wanashriki katika majlisi hizo za maombolezo ya Mjukuu wa Mtume Muhammad SAW, Imam Hussein AS. Kati ya wageni wa heshima wanaoshiriki katika mambolezo hayo ambayo yanafanyika katika siku 10 za kwanza za Mwezi wa Muharram ni Balozi wa Iran nchini Tanzania Mheshimiwa Musa Farhang na mwambata wa utamaduni wa Iran nchini Tanzania Bw. Ali Bagheri na pia Mkuu wa Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Al Mustafa SAW tawi la Tanzania.

Waislamu katika majlisi ya Imam Hussein AS katika Masjid al Ghadeer, Dar es Salaam Tanzania

Hotuba katika majlisi hizo za maombolezo zinatolewa na Sheikh Hemed Jalala Mkuu wa Chuo cha Dini ya Kiislamu cha Imam Swadiq AS mjini Dar es Salaam. Katika hotuba zake, Sheikh Jalala anazungumza kuhusu maisha na shakhsia ya Imam Hussein AS na Hamasa ya Ashura. Aidha msoma mashairi ya maombolezo kutoka Iran ameshiriki katika moja ya vikao hivyo.

Kila mwaka nchini Tanzania wakati wa mwezi wa Muharram, Waislamu hushiriki katika maombolezo ya Imam Hussein AS.