Sep 28, 2017 15:33 UTC
  • Watu watatu wauawa katika shambulio la magaidi wa Boko Haram nchini Nigeria

Maafisa wa Nigeria wameripoti kuwa watu watatu wameuawa katika shambulio lililotekelezwa na kundi la kigaidi la Boko Haram kaskazini mashariki mwa nchi hiyo.

Maafisa wa serikali ya Nigeria wametangaza taarifa hiyo hii leo na kusisitiza kuwa magaidi wa kundi la Boko Haram jana walifanya shambulio katika eneo la kaskazini mashariki mwa nchi ambapo walivamia maghala ya kuhifadhia vyakula ya nyumba 150 na kisha walipora mali na baadaye kuzichoma nyumba hizo katika eneo la Guzamala  jimboni  Borno. 

Nyumba zilizochomwa moto na magaidi wa Boko Haram 

Modu Ganamani afisa wa serikali za mitaa katika eneo la Guzamala ameeleza kuwa, magaidi wa Boko Haram walifika hapo wakiwa wengi kwa kutumia malori na pikipiki na kuanza kutekeleza hujuma huko Goram na katika vijiji viwili jirani vya Lingis na Ajidari. 

Kundi la kigaidi na kitakfiri la Boko Haram lenye makao yake nchini Nigeria hadi kufikia sasa limeuwa watu zaidi ya elfu 20 huko Nigeria, Cameroon, Niger na Chad na kuwafanya wengine zaidi ya milioni mbili kuyahama makazi yao tangu kundi hilo lianzishe hujuma zake mwaka 2009 hadi sasa. 

 

Tags