Wapinzani Kenya waendeleza maandamano ya kutaka mabadiliko katika tume ya uchaguzi
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i35701-wapinzani_kenya_waendeleza_maandamano_ya_kutaka_mabadiliko_katika_tume_ya_uchaguzi
Muungano mkuu wa upinzani Kenya, NASA, leo umeendeleza maandamano ya kutaka mabadiliko katika Tume Huru ya Uchaguzi IEBC.
(last modified 2026-01-14T08:12:18+00:00 )
Oct 15, 2017 11:32 UTC
  • Wapinzani Kenya waendeleza maandamano ya kutaka mabadiliko katika tume ya uchaguzi

Muungano mkuu wa upinzani Kenya, NASA, leo umeendeleza maandamano ya kutaka mabadiliko katika Tume Huru ya Uchaguzi IEBC.

Wapinzani wakiongozwa na mgombea urais kwa tiketi ya NASA Raila Odinga leo wameshiriki katika mkutano wa hadhara mjini Mombasa ambapo wamesistiza kususia uchaguzi wa rais wa marudio Oktoba 26 iwapo hakutakuwa na mabadiliko katika tume ya uchaguzi.

Akihutubia wafuasi wake katika mji huo wa pwani, Odinga amesema katika siku hiyo ya uchaguzi wafuasi wa muungano wa Nasa watashiriki katika maandamano badala ya kupiga kura.

Maandamano ya wapinzani nchini Kenya

Tume ya uchaguzi Kenya IEBC imesema inatekeleza maagizo ya mahakama ya kilele Kenya iliyobatilisha uchaguzi wa Agosti nane baada ya Odinga kulalamikia ushindi wa Rais Uhuru Kenyatta.

Kwa mujibu IEBC, wagombea saba, akiwemo Odinga na Kenyatta wanatazamiwa kuwa katika makaratasi ya kupiga kura ingawa Odinga ameandika barua ya kujiondoa katika mchuano huo.