RSF: Waandishi habari wanakandamizwa katika nchi za Afrika
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i36116-rsf_waandishi_habari_wanakandamizwa_katika_nchi_za_afrika
Shirika la Maripota Wasio na Mpaka (RSF) limetahadharisha kuhusu hali ya mbaya ya waandishi habari katika baadhi ya nchi za Afrika.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Nov 02, 2017 14:09 UTC
  • RSF: Waandishi habari wanakandamizwa katika nchi za Afrika

Shirika la Maripota Wasio na Mpaka (RSF) limetahadharisha kuhusu hali ya mbaya ya waandishi habari katika baadhi ya nchi za Afrika.

Shirika hilo limetangaza kuwa, waandishi habari katika baadhi ya nchi za Kiafrika hawana uhuru wa kujieleza na wanafanya kazi katika mazingira ya mashinikizo na ukandamizaji.

Shirika la Maripota Wasio na Mpaka limesema kuwa, waandishi habari katika nchi ya Libya wanasumbuliwa na aina mbalimbali za mashinikizo, vitisho na kutekwa nyara kutokana na hali ya ukosefu wa utulivu wa kisiasa, mapigano kati ya makundi hasimu na harakati za makundi ya kigaidi katika maeneo mbalimbali ya nchi hiyo. 

Waandishi habari wanauawa Libya

Shirika hilo pia limeashiria hali ya waandishi wa habari katika nchi ya Guinea Conakry na kusema waandishi bahari wanaopinga ukati na ukiukwaji wa uhuru wa kusema nchini humo wanatiwa nguvuni, kunyanyaswa na kupigwa. 

Ripoti ya Shirika la Maripota Wasio na Mpaka pia limeashiria hali ya waandishi habari katika nchi nyingine za Afrika kama Mali na kusema waandishi hao hawana usalama na amani. 

Tarehe Pili Novemba imepewa jina la Siku ya Kimataifa ya Kukomesha Ukatili dhidi ya Wandishi wa Habari.