UNICEF yaeleza wasiwasi wake kuhusu ukatili unaofanywa dhidi ya watoto duniani
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i36117-unicef_yaeleza_wasiwasi_wake_kuhusu_ukatili_unaofanywa_dhidi_ya_watoto_duniani
Afisa wa Shirika la Watoto la Umoja wa Mataifa (UNICEF) ametangaza kuwa, karibu watoto milioni 300 wanakabiliwa na ukatili na manyanyaso kote duniani.
(last modified 2023-11-27T12:14:11+00:00 )
Nov 02, 2017 17:40 UTC
  • UNICEF yaeleza wasiwasi wake kuhusu ukatili unaofanywa dhidi ya watoto duniani

Afisa wa Shirika la Watoto la Umoja wa Mataifa (UNICEF) ametangaza kuwa, karibu watoto milioni 300 wanakabiliwa na ukatili na manyanyaso kote duniani.

Cornelius Williams amesema kuwa, mienendo mibaya na unyanyasaji unaofanyika dhidi ya watoto katika maeneo mbalimbali ya dunia unasababish madhara makubwa kwa watoto hao. 

Ripoti mbalimbali za Shirika la Watoto la Umoja wa Mataifa zimesema kuwa karibu asilimia 60 ya watoto wenye umri wa mwaka mmoja katika nchi 30 wanakabiliwa na ukatili na kwamba robo yao wanachapwa na kupigwa. 

Ripoti hiyo imesema kuwa, wasichana milioni 15 wenye umri wa kati ya miaka 15 hadi 19 kote duniani wamelazimishwa kufanya ngono. 

UNICEF pia imeashiria manyanyaso na ukatili unaofanyika dhidi ya Wamarekani weusi na kusisitiza kuwa, idadi ya vijana wa Marekani weusi wanaouawa kila mwaka ni mara 19 zaidi ya wenzao wazungu. 

Vilevile takwimu zinaonesha kuwa robo tatu ya vitendo vya mashambulizi ya risasi mashuleni katika kipindi cha miaka 25 iliyopita vimetokea nchini Marekani.