SAUTI, Kampuni ya RAHCO Tanzania, yatakiwa kuwalipa wananchi waliobomolewa nyumba zao Dar
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i36260-sauti_kampuni_ya_rahco_tanzania_yatakiwa_kuwalipa_wananchi_waliobomolewa_nyumba_zao_dar
Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora nchini Tanzania, imetoa maamuzi ya malalamiko ya wakazi 72 wa kata ya Mnyamani, Vingunguti jijini Dar es Salaam kulipwa fidia kufuatia nyumba zao kubomolewa.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Nov 08, 2017 12:56 UTC

Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora nchini Tanzania, imetoa maamuzi ya malalamiko ya wakazi 72 wa kata ya Mnyamani, Vingunguti jijini Dar es Salaam kulipwa fidia kufuatia nyumba zao kubomolewa.

Kadhalika tume hiyo imeitaka kampuni hodhi ya rasilimali za reli nchini humo 'RAHCO' iliyohusika na bomoabomoa hiyo kuheshimu misingi ya ubinaadamu huku ikililalamikia jeshi la polisi kwa kutumia nguvu katika zoezi hilo.

Bomoabomoa ikiendelea kando ya reli

Hii ni baada ya bomoabomoa jijini hapo kushika kasi katika kipindi cha miezi ya hivi karibuni, suala ambalo limeibua malalamiko mengi ya waathiriwa ambao inadaiwa kuwa huwa hawalipwi fidia na mamlaka husika.

Mwandishi wetu Silvano Kayera wa jijini Dar es Salaam Tanzania ametuandalia ripoti kamili........../