Nov 26, 2017 07:53 UTC
  • Boko Haram yatwaa mji katika jimbo la Borno

Kundi la kigaidi la Boko Haram limeutwaa mji mmoja katika jimbo la Borno kaskazini mashariki mwa Nigeria. Wakazi wa mji wa Magumeri wamesema kuwa magaidi wa kitakfiri jana waliingia katika mji huo yapata umbali wa kilomita 50 kutoka makao makuu ya Maiduguri.

Baada ya kuingia katika mji huo, magaidi wa Boko Haram walianza  kuwafyatulia risasi raia na kuwarushia mada za milipuko, hatua ambayo iliwalazimisha wakazi wa wake kukimbilia katika misitu jirani.

Uvamizi huo wa magaidi wa kundi la Boko Haram umefanyika siku chache baada ya mlipuko wa bomu kuuwa watu wasiopungua 50 msikitini katika jimbo jirani la Adamawa.

Shambulio la Boko Haram lililouwa watu wasiopungua 50 msikitini  

 

Watu zaidi ya 20,000 wameuawa hadi sasa tangu kundi la Boko Haram lianzishe mashambulizi na hujuma zake za kikatili huko kaskazini mashariki mwa Nigeria mwaka 2009.  Hujuma hizo za Boko Haram zimesaabisha vifo vingi pia katika nchi jirani za Chad, Niger na Cameroon.

Tags