Wanajeshi wa Italia walio Iraq kupelekwa Niger
(last modified Mon, 25 Dec 2017 06:51:13 GMT )
Dec 25, 2017 06:51 UTC
  • Wanajeshi wa Italia walio Iraq kupelekwa Niger

Waziri Mkuu wa Italia Paolo Gentilon amesema atapendekeza katika bunge la nchi hiyo kuwa baadhi ya wanajeshi wa Italia walio Iraq wapelekwe Niger kupambana na biashara haramu ya usafirishaji binadamu na ugaidi.

Gnetiloni amesema wanajeshi 1,400 wa Italia walio Iraq wanaweza kupunguzwa kufuatia mafanikio ya hivi karibuni dhidi ya kundi la kigaidi la ISIS nchini humo. Amesema hivi sasa kuna haja ya kutuma askari zaidi katika eneo la Sahel la Afrika Magharibi.

Duru za habari nchini Italia zinasema askari hao ni kati ya ahadi alizotoa Gnetiloni kwa Rais Emmanuel Macron wa Ufanrasa ambaye amesema nchi yake itatuma idadi kubwa ya askari katika eneo la Sahel linalojumuisha nchi za kundi la G5 ambazo ni Mali, Mauritania, Niger,Burkina Faso na Chad.

Wanajeshi wa Italia

Kikosi hicho kimepanga kuendesha doria katika eneo la Sahel kwa kushirikiana na wanajeshi 4000 wa Ufaransa waliotumwa katika eneo hilo.

Kundi la kigaidi la Boko Haram limekuwa likitekeleza hujuma katika baadhi ya nchi za Sahel. Aidha inaaminika kuwa magaidi wanafungamana na mtandao wa al Qaeda wamejizatiti katika eneo hilo. Nchi hizo za Sahel pia ni chanzo cha maelfu ya wahajiri haramu wa Kiafrika wanaokimbilia bara Ulaya kila siku,

Tags