Italia yaidhinisha kutuma wanajeshi Niger, na vikosi zaidi kaskazini mwa Afrika
(last modified Thu, 18 Jan 2018 07:55:02 GMT )
Jan 18, 2018 07:55 UTC
  • Italia yaidhinisha kutuma wanajeshi Niger, na vikosi zaidi kaskazini mwa Afrika

Bunge la Italia jana liliidhinisha kuongezwa idadi ya wanajeshi wake huko Libya na kutumwa wanajeshi wa nchi hiyo hadi 470 huko Niger kwa ajili ya kukomesha harakati za wahajiri na magendo ya binadamu kuelekea Ulaya.

Mwishoni mwa mwaka jana, Waziri Mkuu wa Italia Paolo Gentiloni alisema kuwa atatuma tena wanajeshi wa nchi hiyo kaskazini mwa Afrika ambao watatoka Iraq na Afghanistan.

Paolo gentiloni, Waziri Mkuu wa Italia 

Mwaka huu wa 2018 Italia imepanga kutumia yuro bilioni 1.5 kwa ajili ya vikosi vyake vya kijeshi katika nchi 21 duniani. Hadi sasa ni sehemu tu ya bajeti hiyo ambayo tayari imeidhinishwa. Italia imeamua kujielekeza zaidi barani Afrika ikiwa ni katika jitihada za kuwazuia wahamiaji kufika katika pwani za nchi hiyo. Wahajiri wengi wa Kiafrika kwanza huvuka nchi za eneo la Sahel ili kuweza kufika Libya; na baada ya hapo hujipakiza botini na kuanza safari kuelekea Italia. Wahajiri wa Kiafrika zaidi ya laki sita wamewasili Italia katika kipindi cha miaka minne iliyopita. 

Wahajiri wa Kiafrika baada ya kuwasili katika mji wa Sicily Italia 
 

Tags