UN yatahadharisha kuhusu hali ya wakimbizi Libya
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i40979-un_yatahadharisha_kuhusu_hali_ya_wakimbizi_libya
Mratibu wa Masuala ya Kibinadamu wa Umoja wa Mataifa ametahadharisha kuhusu hali ya kusikitisha ya wakimbizi walioko Libya.
(last modified 2023-11-27T12:14:11+00:00 )
Feb 28, 2018 16:26 UTC
  • UN yatahadharisha kuhusu hali ya wakimbizi Libya

Mratibu wa Masuala ya Kibinadamu wa Umoja wa Mataifa ametahadharisha kuhusu hali ya kusikitisha ya wakimbizi walioko Libya.

Taarifa iliyotolewa na Maria Ribeiro imesema kuwa, zaidi ya raia laki moja na 80 elfu wa Libya waliokimbia machafuko na ukosefu wa usalama wanahitajia misaada ya kibinadamu.

Maria Ribeiro ameongeza kuwa, wakimbizi wengine laki tatu na 35 elfu waliorejea hivi karibuni katika miji na vijiji vyao wangali wanahitajia misaada. 

Mratibu wa Masuala ya Kibinadamu wa Umoja wa Mataifa nchini Libya amesema kuwa, mbali na idadi hiyo kubwa ya wakimbizi wa Kilibya, maelfu ya wahajiri haramu pia kutoka nchi zilizokumbwa na migogoro ya vita barani Afrika wamekimbilia nchini humo. 

Wahajiri wanauzwa kama bidhaa nchini Libya

Makundi ya kutetea haki za binadamu yanasema kuwa, kwa sasa zaidi ya wakimbizi na wahajiri haramu elfu 17 wanashikiliwa katika korokoro za nchi hiyo na maelfu ya wengine wanashikiliwa na magenge ya magendo ya binadamu.