ICCN: Waasi wengi Kongo DR wanaendesha harakati zao katika msitu wa Virunga
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i4312-iccn_waasi_wengi_kongo_dr_wanaendesha_harakati_zao_katika_msitu_wa_virunga
Taasisi ya hifadhi ya maliasili nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, imeutaja msiti wa Virunga kuwa unaoongoza kwa machafuko yanayotokana na wanamgambo mbalimbali wa waasi nchini humo.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Apr 02, 2016 21:51 UTC
  • ICCN: Waasi wengi Kongo DR wanaendesha harakati zao katika msitu wa Virunga

Taasisi ya hifadhi ya maliasili nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, imeutaja msiti wa Virunga kuwa unaoongoza kwa machafuko yanayotokana na wanamgambo mbalimbali wa waasi nchini humo.

Taasisi hiyi ya ICCN (Institut Congolais pour la Conservation de la Nature) imelaani uvamizi usio wa kisheria wa wanamgambo wa waasi dhidi ya hifadhi ya wanyama ya Virunga na kuongeza kuwa, hatua ya kuwaweka wakimbizi wa Kihutu katika eneo hilo, imechangia kuharibu hali ya mambo zaidi. ICCN imeashiria operesheni za jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kwa kushirikiana na askari wa wanyamapori wa hifadhi ya Virunga kwa ajili ya kuhitimisha uvamizi usio wa kisheria dhidi ya mbuga hiyo ya wanyama katika kipindi cha siku 15 zilizopita, na kusema kuwa, suala hilo litazusha ushindani wa kisiasa na migogoro ya kikaumu nchini humo. Meya wa mkoa wa Kivu Kaskazini, Jules Hakizumwami amesema kuwa, maelfu ya wakazi wa eneo la Kigaligali, katika mkoa huo wameyaacha makazi na mashamba yao na kukimbilia maeneo mengine, amesema kuwa, raia hao wa eneo hilo wamelazimika kuwa wakimbizi kutokana na uwepo wa wakimbizi wa Kihutu na waasi wa Kihutu kutoka Rwanda. Itakumbukwa kuwa eneo la mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo limekuwa katika hali ya machafuko kwa kipindi cha miaka 20 sasa, kutokana na harakati za wanamgambo wenye silaha.