Magaidi 21 waangamizwa Rasi ya Sinai nchini Misri
(last modified Thu, 10 May 2018 13:47:46 GMT )
May 10, 2018 13:47 UTC
  • Magaidi 21 waangamizwa Rasi ya Sinai nchini Misri

Jeshi la Misri limetangaza habari ya kuangamizwa magaidi 21 katika operesheni ya pamoja iliyofanywa na jeshi na polisi wa nchi hiyo katika Rasi ya Sinai.

Jeshi la Misri limesema, watu wengine 238 wametiwa mbaroni katika operesheni ya jeshi na polisi wa Misri kwenye eneo la Sinai katika siku za hivi karibuni.

Taarifa ya jeshi la Misri imefafanua kuwa, magaidi 259 wameshauwa tangu ilipoanza operesheni hiyo na watu 4467 wameshatiwa mbaroni.

Magaidi wa Daesh (ISIS) hawaheshimu hata nyumba za ibada. Baadhi ya picha za mauaji ya kutisha yaliyofanywa na magaidi hao ndani ya msikiti

 

Mwezi Fefruari mwaka huu, jeshi la Misri kwa kushirikiana na polisi walizanisha opesheni ya pamoja inayojulikana kwa jina la Sinai 2018  kwa shabaha ya kuyasafisha magenge ya kigaidi katika eneo hilo la kaskazini mwa nchi hiyo.

Wakati huo huo shirika la haki za binadamu la Human Rights Watch hivi karibuni lilitahadharisha kuhusu uwezekano wa kutokea mgogoro wa kibinadamu katika Rasi ya Sinai, kaskazini mwa Misri.

Rasi ya Sinai huko Misri ni makao makuu ya magenge ya kigaidi likiwemo tawi la kundi la wakufurishaji la Daesh (ISIS) na limekuwa uwanja wa mapigano na mashambulizi ya kigaidi kwa miaka kadhaa sasa.

Tags