AU yampinga vikali Trump na kutangaza kuiunga mkono kikamilifu JCPOA
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i44304-au_yampinga_vikali_trump_na_kutangaza_kuiunga_mkono_kikamilifu_jcpoa
Mkuu wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika ameelezea wasiwasi wake kutokana na uamuzi wa serikali ya Marekani wa kujitoa katika mapatano ya nyuklia ya JCPOA na kusema AU inaunga mkono kikamilifu mapatano hayo ya kimataifa.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
May 10, 2018 10:13 UTC
  • AU yampinga vikali Trump na kutangaza kuiunga mkono kikamilifu JCPOA

Mkuu wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika ameelezea wasiwasi wake kutokana na uamuzi wa serikali ya Marekani wa kujitoa katika mapatano ya nyuklia ya JCPOA na kusema AU inaunga mkono kikamilifu mapatano hayo ya kimataifa.

Moussa Faki amesema hayo leo ameongeza kuwa, Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomikini IAEA umetangaza mara nyingi kuwa Iran imeheshimu kikamilifu mapatano hayo na kusisitiza kuwa, mapatano ya kimataifa ya JCPOA yamepasishwa kwa kaulki moja na Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa.

Mkuu huyo wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika ameongeza kuwa, uamuzi wa rais wa Marekani Donald Trump wa kujitoa katika mapatano ya JCPOA umeandaa uwanja wa kuongezeka machafuko katika eneo hili na kutia doa itibari ya kuheshimiwa mapatano ya kimataifa.

Ndani ya jengo la Makao Makuu ya Umoja wa Afrika mjini Addis Ababa Ethiopia

 

Jumanne usiku Donald Trump alitangaza kuitoa Marekani katika mapatano ya nyuklia ya JCPOA licha ya nchi yake kushiriki kikamilifu katika kuyafanikisha.

Hatua hiyo ya upande mmoja ya Marekani imedharau juhudi zote za miaka 12 za kidiplomasia zilizopelekea kupatikana mapatano hayo ambayo yana baraka kamili za Umoja wa Mataifa kasma ambavyo kitendo hicho cha Trump kinahesabiwa kuwa ni jeuri za wazi na ni dharau kubwa kwa pande nyingine zilizofanikisha mapatano hayo.