Magaidi 19 wauawa na jeshi la Misri katika eneo la Sinai
Jeshi la Misri limetangaza habari ya kuangamizwa magaidi 19 katika operesheni iliyofanywa na jeshi la nchi hiyo katika Peninsula ya Sinai.
Taarifa ya jeshi la nchi hiyo imesema magaidi hao wameangamizwa katika operesheni iliyofanywa na jeshi hilo katika maeneo ya katikati na kaskazini mwa nchi.
Wiki iliyopita, magaidi wengine 21 waliuawa katika operesheni ya pamoja iliyofanywa na jeshi na polisi wa nchi hiyo katika Rasi ya Sinai, mbali na wengine 238 kutiwa mbaroni.
Duru za habari zimeeleza kuwa, magaidi wasiopungua 280 wameshauwa tangu ilipoanza operesheni hiyo, na watu 4467 wameshatiwa mbaroni. Kadhalika jeshi la Misri limepoteza askari wake wapatao 33 katika operesheni hiyo.
Mwezi Februari mwaka huu, jeshi la Misri kwa kushirikiana na polisi lilianzisha operesheni ya pamoja inayojulikana kwa jina la 'Sinai 2018' kwa shabaha ya kuyasafisha magenge ya kigaidi katika eneo hilo la kaskazini mwa nchi.