UN: Wafanya magendo ya binadamu waua wahajiri 12 Libya
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i45274-un_wafanya_magendo_ya_binadamu_waua_wahajiri_12_libya
Umoja wa Mataifa umesema wahajiri 12 wameuawa kwa kupigwa risasi na wafanya magendo ya binadamu, walipokuwa wakijirabu kukimbia kambini nchini Libya.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jun 01, 2018 09:23 UTC
  • UN: Wafanya magendo ya binadamu waua wahajiri 12 Libya

Umoja wa Mataifa umesema wahajiri 12 wameuawa kwa kupigwa risasi na wafanya magendo ya binadamu, walipokuwa wakijirabu kukimbia kambini nchini Libya.

Shirika la Kuhudumia Wakimbizi la Umoja wa Mataifa UHNCR limesema leo Ijumaa kuwa, wahajiri hao waliuawa wiki iliyopita (Mei 23), baada ya kundi la wahajiri 200 kujajaribu kutoroka katika kambi moja walikokuwa wameshikwa mateka katika mji wa Bani Walid, ulioko yapata kilomita 170 kusini mashariki mwa Tripoli.

UNHCR imenukuu taarifa ya Jumuiya ya Madaktari Wasio na Mipaka ikisema kuwa, Idara ya Uhamiaji ya Libya kwa kushirikiana na Shirika la Kimataifa la Wahamiaji imefanikiwa kuwarejesha nyumbani kwa ndege raia 163 wa Somalia wengine 30 raia wa Bangladesh na 28 raia wa Pakistan waliokuwa wanaishi nchini Libya kinyume cha sheria.

Wahajiri wa Kiafrika nchini Libya

Libya ni kituo kikuu cha wahamiaji haramu hasa wa Kiafrika wanaokimbilia barani Ulaya. Hata hivyo kuna idadi kubwa pia ya wahajiri kutoka nchi nyingine kama za Mashariki ya Kati na magharibi mwa Asia ambao nao wanaitumia Libya katika kituo kikuu cha kwenda kutafuta maisha barani Ulaya.

Magenge ya kigaidi na ya magendo ya binadamu yanatumia ukosefu wa amani na kutokuweko serikali kuu yenye nguvu nchini Libya kufanya uhalifu huo.