Iran na Kongo DR, wahanga wa propaganda za vyombo vya habari
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i45410-iran_na_kongo_dr_wahanga_wa_propaganda_za_vyombo_vya_habari
Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Vyombo vya Habari katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (ACP) ametoa mwito wa kuimarishwa uhusiano wa nchi yake na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika kupambana na propaganda za maadui dhidi ya nchi mbili hizo.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jun 04, 2018 10:15 UTC
  • Iran na Kongo DR, wahanga wa propaganda za vyombo vya habari

Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Vyombo vya Habari katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (ACP) ametoa mwito wa kuimarishwa uhusiano wa nchi yake na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika kupambana na propaganda za maadui dhidi ya nchi mbili hizo.

Lambert Kaboyi ametoa mwito huo katika mkutano wake na Jahanbakhsh Hasanzadeh, Balozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran nchini Kongo na kuongeza kuwa, maadui wa Kongo DR na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran wanatumia njia za kila namna kupotosha ukweli katika vyombo vya habari ili kuzisababishia madhara nchi mbili hizo.

Amesisita kuwa, kwa msingi huo Tehran na Kinshasa zinapaswa kuimarisha uhusiano wao katika uga wa vyombo vya habari ili kukabiliana na propaganda hizo.

Baadhi ya magazeti yanayochapishwa katika nchi za Afrika

Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Vyombo vya Habari katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kadhalika amebainisha kuwa, kwa vile Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imepiga hatua na kujiimarisha katika sekta ya uanahabari, kuna umuhimu kwa waandishi wa habari wa DRC kujifunza na kustafidi na uzoefu huo wa Iran.

Kwa upande wake, Jahanbakhsh Hasanzadeh, Balozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuna haja nchi mbili hizi ziimarishe uhusiano na ushirikiano wao katika uga wa vyombo vya habari, ili kushinda njama hizo za maadui wa nchi mbili hizi.