Maandamano dhidi ya serikali yafanyika Ghana
Wananchi wa Ghana wameandamana katika mji wa katikati mwa nchi hiyo dhidi ya serikali.
Maelfu ya wananchi wa Ghana jana walimiminika katika mitaa mbalimbali ya mji wa Kumasi yapata umbali wa kilomita 270 kaskazini magharibi mwa Accra mji mkuu wa nchi hiyo katika mkoa wa Ashanti wakipinga siasa za Tume ya Uchaguzi ya nchi hiyo za kukaidi mapendekezo ya kuhalalisha ustahiki wa wagombea kabla ya kufanyika uchaguzi mkuu wa mwaka huu.
Maandamano hayo yaliitishwa na makundi kwa jina la Let My Vote Count Alliance and Alliance for Accountable Governance, na kuhudhuriwa pakubwa na wanachama wa chama kikuu cha upinzani cha New Patriotic ambacho pia kinataka kufanyika marebisho hayo.
Wafanya maandamano hao katika mji wa Kumasi wametaka kufanyiwa marekebisho siasa za uchaguzi nchini humo. Waandamanaji hao wametangaza kuwa hawataacha kufanya juhudi za kutaka marekebisho hadi pale Tume ya Uchaguzi ya nchi hiyo itakapoheshimu sheria.