Hali ya hatari yarefushwa nchini Misri
(last modified Mon, 25 Jun 2018 02:54:04 GMT )
Jun 25, 2018 02:54 UTC
  • Hali ya hatari yarefushwa nchini Misri

Bunge la Misri kwa mara ya nne limeongeza muda wa hali ya hatari kwa miezi mingine mitatu.

Zaidi ya theluthi moja ya wabunge wa Misri wameafiki ombi la Rais Abdel Fattah el Sisi wa nchi hiyo la kuongeza muda wa hali ya hatari kwa mara ya nne; hali ambayo ilianza kutekelezwa tangu mwezi Aprili mwaka jana. 

Mripuko kanisani Misri 

Hali ya hatari  ilitangazwa kwa mara ya kwanza nchini Misri mwezi Aprili mwaka jana na ikaanza kutekelezwa baada ya kutokea miripuko ya mabomu katika makanisa mawili nchini humo iliyouwa watu wasiopungua 45. Aidha hali hiyo ya hatari iliongezewa muda mwezi Julai na Oktoba mwaka jana na vile vile mwezi Januari mwaka huu. 

Serikali ya Misri inadai kuwa inatekeleza hali hiyo ya hatari lengo likiwa ni kupambana na ugaidi. Kwa upande wake taasisi za kutetea haki za binadamu zimeitahadharisha serikali ya Cairo kuwa haki za raia zinakanyagwa na kubinywa kufuatia kutekelezwa hali ya hatari huko Misri. 

Tags