Jul 08, 2018 07:45 UTC
  • Riek Machar kurejeshwa katika nafasi ya Makamu wa Rais wa Sudan Kusini

Pande hasimu Sudan Kusini zimeafiki kugawana madaraka kwa mujibu wa makubaliano yaliyofikiwa na pande hizo ambapo kwa mujibu wake kiongozi wa waasi nchini humo, Riek Machar atarejeshwa katika wadhifa wa Makamu wa Rais.

Al Dierdiry Ahmed  Waziri wa Mambo ya Nje wa Sudan alisema jana kuwa imeafikiwa kwamba kutakuwepo makamu wanne wa rais; yaani makamu wawili wa rais waliopo hivi sasa pamoja na Riek Machar, na nafasi ya nne ya makamu wa rais atapangiwa mwanamama kutoka kambi ya upinzani.

Itakumbukwa kuwa mrengo wa upinzani nchini Sudan Kusini na serikali ya nchi hiyo wamefikia makubaliano huko Kampala mji mkuu wa Uganda katika juhudi za kuhitimisha vita vya ndani nchini Sudan Kusini. Vita hivyo vilianza mwaka 2013 baada ya hitilafu za kisiasa kati ya Rais Salva Kiir na aliyekuwa makamu wake, Machar kusababisha machafuko ya ndani.  

Rais Salva Kiir, Rais al Bashir na Riek Machar katika mazungumzo ya kusaka amani 

Pande mbili hizo hasimu nchini Sudan Kusini zimehusika katika mauaji ya ulipizaji kisasi ambayo yaliibua miganyiko ya kikabila. Makumi ya maelfu ya watu wameuawa na mamilioni ya wengine kuwa wakimbizi kufuatia machafuko hayo.

Tags