Maandamano yaendelea Nigeria kutaka Sheikh Zakzaky aachiliwe huru
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i46643-maandamano_yaendelea_nigeria_kutaka_sheikh_zakzaky_aachiliwe_huru
Wananchi wameendelea kuandamana katika mji mkuu wa Nigeria, Abuja wakitaka serikali ya hiyo imuahcilie huru Sheikh Ibrahim Zakzaky kiongozi wa harakati ya Kiislamu nchini humo.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jul 08, 2018 08:57 UTC
  • Maandamano yaendelea Nigeria kutaka Sheikh Zakzaky aachiliwe huru

Wananchi wameendelea kuandamana katika mji mkuu wa Nigeria, Abuja wakitaka serikali ya hiyo imuahcilie huru Sheikh Ibrahim Zakzaky kiongozi wa harakati ya Kiislamu nchini humo.

Maandamano hayo hayo mapya ni msururu wa maandamano ya karibu kila siku ambayo yalishika kasi Juni 14 wakati Mahakama ya Jimbo la Kaduna ilipoahirisha kesi ya Sheikh Zakzaky hadi Julai 13.

Taarifa zinasema tokea wakati huo hadi sasa watu 42 wameuawa kwa kufyatiliwa risasi na askari wa Nigeria wakati wa maandamano ya amani ya kutaka Sheikh Zakky aachiliwe huru huku mamia ya wengine wakikamatwa.

Ikumbukwe kuwa Sheikh Ibrahim Zakzaky, mkuu wa Harakati ya Kiislamu ya Nigeria alikamtwa baada ya kupigwa risasi na kujeruhiwa vibaya yeye na mke wake mwezi Disemba 2015 wakati jeshi la nchi hiyo lilipovamia Husainia ya Baqiyyatullah mjini Zaria na kuua kwa umati mamia ya Waislamu.

Waandamanji wanaotaka Sheikh Zakzaky aachiliwe huru wakishambuliwa kwa gesi ya kutoa machozi na polisi  mjini Abuja

Watoto wa Sheikh Zakzkay ni miongoni mwa mamia ya Waislamu waliouliwa shahidi na  kujeruhiwa na wanajeshi wa Nigeria katika jinai hiyo.

Hivi sasa miaka miwili na nusu imepita tangu kutokea uvamizi huo lakini serikali ya Nigeria ingali inang'ang'ania kumshikilia korokoroni Sheikh Ibrahim Zakzaky licha ya kuwa mwaka 2016 Mahakama Kuu ya nchi hiyo ilitoa amri ya kuachiliwa huru.