SAUTI, Waislamu nchini Kenya wapinga uteuzi wa mabalozi Wakristo kupelekwa maeneo matukufu
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i47104-sauti_waislamu_nchini_kenya_wapinga_uteuzi_wa_mabalozi_wakristo_kupelekwa_maeneo_matukufu
Waislamu nchini Kenya wamemtaka Rais Uhuru Kenyatta wa nchi hiyo kuwa makini katika kuzingatia maeneo anayowatuma mabalozi wake duniani.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jul 29, 2018 12:15 UTC

Waislamu nchini Kenya wamemtaka Rais Uhuru Kenyatta wa nchi hiyo kuwa makini katika kuzingatia maeneo anayowatuma mabalozi wake duniani.

Hatua hiyo imekuja baada ya rais huyo kumteua Mkristo kuwa balozi wa Saudi Arabia, kitendo ambacho kimepingwa vikali na Waislamu hao ambao wamemtaka Kenyatta, kutengua uteuzi huo na badala yake kumuainisha Mwislamu mahala hapo.

Rais Uhuru Kenyetta wa Kenya

Aidha Waislamu hao wamehoji kwamba itakuwaje iwapo Mkenya aliye mjini Makkah au Madina atapata tatizo na kisha ikahitajika balozi wa nchi hiyo aende kukutana na Mkenya huyo, hasa kwa kuzingatia kuwa watu wasiokuwa Waislamu hawaruhusiwi kufika maeneo hayo? Ni kwa ajili hiyo wametangaza kuitisha kampeni ya kuwashawishi viongozi wa serikali ili wamshauri Rais Kenyatta abadili uamuzi wake.

Tujiunge na mwandishi wetu wa mjini Mombasa, Seifullah Murtadha kwa taarifa kamili………./