Askari wa Misri waliotekwa nyara Libya wakombolewa
(last modified Tue, 31 Jul 2018 13:45:38 GMT )
Jul 31, 2018 13:45 UTC
  • Askari wa Misri waliotekwa nyara Libya wakombolewa

Maafisa usalama wa Sudan wametangaza kuwa wanajeshi wa Misri waliokuwa wametekwa nyara katika mpaka wa kusini mwa Libya wamekombolewa.

Waafisa wa usalama wa Sudan wametangaza leo kuwa kundi la wanajeshi wa Misri waliokuwa wametekwa nyara na kundi moja la waasi wa Libya Limekombolewa. Taarifa ya maafisa hao imesema kuwa, askari watano wa Misri akimo afisa mmoja wa ngazi za juu jeshini wamekombolewa katika operesheni iliyofanyika kusini mwa Libya.

Askari hao wa Misri walitekwa nyara katika eneo la mpaka wa Misri, Libya na Sudan na walikuwa njiani kupelekwa ndani ya Libya. 

Mkuu wa vyombo vya usalama vya Sudan, Salah Abdallah Gosh ndiye aliyesimamia operesheni ya kukomboa wanajeshi hao wa Misri. 

Sudan imechukua hatua hiyo licha ya kwamba inahitilafiana na Misri katika masuala kadhaa ikiwa ni pamoja na mgogoro wa nchi hizo mbili kuhusu umiliki wa maeneo ya Halayib na Shalateen na hitilafu za pande mbili kuhusu bwawa linalojengwa na Ethiopia juu ya maji ya mto Nile. 

Tags