Mahakama ya Kaduna kusikiliza kesi ya Sheikh Zakzaky Oktoba 4
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i47217-mahakama_ya_kaduna_kusikiliza_kesi_ya_sheikh_zakzaky_oktoba_4
Mahakama Kuu ya jimbo la Kaduna nchini Nigeria imetangaza kuwa, itasikiliza ombi la kuachiliwa huru kwa dhamana Sheikh Ibrahim Zakzaky, Kiongozi wa Harakati ya Kkiislamu ya Nigeria.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Aug 03, 2018 23:52 UTC
  • Mahakama ya Kaduna kusikiliza kesi ya  Sheikh Zakzaky Oktoba 4

Mahakama Kuu ya jimbo la Kaduna nchini Nigeria imetangaza kuwa, itasikiliza ombi la kuachiliwa huru kwa dhamana Sheikh Ibrahim Zakzaky, Kiongozi wa Harakati ya Kkiislamu ya Nigeria.

Taarifa ya mahakama hiyo imeeleza kuwa, tarehe 4 Oktoba mwaka huu itakuwa siku ya kusikiliza ombi la kuachiliwa huru kwa dhamana Sheikh Ibrahim Zakzaky pamoja na mkewe kufuatia ombi lililowasilishwa na mawakili wao.

Maxwel Keon, mmoja wa mawakili wa Sheikh Zakzaky amesema kuwa, wana matumaini mteja wao ataachiliwa huru kwa dhamana. 

Sheikh Ibrahim Zakzaky, Mkuu wa Harakati ya Kiislamu ya Nigeria alikamatwa baada ya kupigwa risasi na kujeruhiwa vibaya yeye na mke wake mwezi Disemba 2015 wakati jeshi la nchi hiyo lilipovamia Husainia ya Baqiyyatullah mjini Zaria na kuua kwa umati mamia ya Waislamu.

Maandamano ya kutaka kuachiliwa huru Sheikh Ibrahim Zakzaky

Hivi sasa miaka miwili na nusu imepita tangu kutokea uvamizi huo, lakini serikali ya Nigeria ingali inang'ang'ania kumshikilia korokoroni Sheikh Ibrahim Zakzaky licha ya kuwa mwaka 2016 Mahakama Kuu ya nchi hiyo ilitoa amri ya kuachiliwa huru mwanaharakati huyo wa Kiislamu.

Hivi karibuni, Mahakama Kuu ya jimbo la Kaduna iliwaachilia huru wafuasi wa Harakati ya Kiislamu ya Nigeria inayoongozwa na Sheikh Ibrahim Zakzaky ambaye angali anashikiliwa na vyombo vya usalama vya nchi hiyo, hatua ambayo imeleta matumaini ya kufutiwa mashataka pia mwanaharakati huyo wa Kiislamu.