UN yaiwekea Libya vikwazo kwa ukatili wa kingono
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i49328-un_yaiwekea_libya_vikwazo_kwa_ukatili_wa_kingono
Umoja wa Mataifa umezidisha vikwazo dhidi ya nchi ya Libya kutokana na kesi nyingi za ubakaji na ukatili wa kingono zilizoripotiwa nchini humo.
(last modified 2026-02-21T22:51:18+00:00 )
Nov 06, 2018 10:06 UTC
  • UN yaiwekea Libya vikwazo kwa ukatili wa kingono

Umoja wa Mataifa umezidisha vikwazo dhidi ya nchi ya Libya kutokana na kesi nyingi za ubakaji na ukatili wa kingono zilizoripotiwa nchini humo.

Wanachama wote wa Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa wamepasisha muswada wa kuzidisha vikwazo dhidi ya Libya isipokuwa Russia na China ambazo hazikushiriki katika zoezi hilo. 

Azimio hilo la Baraza la Usalama linatayarisha njia ya kuzidishwa vikwazo vya Libya kutokana na kesi nyingi za ubakaji na ukatili wa kingono zinazoripotiwa nchini humo. 

Wahajiri wanabakwa na kunajisiwa Libya.

Mwakilishi wa Russia katika Umoja wa Mataifa, Vasily Nebenzya amesema ubakaji na ukatili wa kingono vinatambuliwa kuwa ni uhalifu na makosa ya jinai katika kila nchi lakini Moscow inaona kuwa, masuala hayo yalipaswa kujadiliwa katika Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa na si katika Baraza la Usalama linaloshughulikia vitisho vya usalama wa kimataifa. Nebenzya ameongeza kuwa, baadhi ya nchi za Ulaya zinatumia vibaya suala hilo kwa maslahi yao ya kisiasa. 

Maafisa wa Umoja wa Mataifa wametahadharisha kuwa, wanachama wa makundi ya waasi, wafanya magendo ya wahajiri na magenge ya wahalifu yamekuwa yakifanya jinai za ubakaji na ukatili wa ngono kwa kiasi kikubwa katika nchi ya Liibya ambayo ilitumbukia katika ghasia na machafuko baada ya kuondolewa madarakani kiongozi wa zamani wa nchi hiyo, Muammar Gaddafi mwaka 2011.