Kongo na Iran kuimarisha ushirikiano wao katika uga wa habari
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i49490-kongo_na_iran_kuimarisha_ushirikiano_wao_katika_uga_wa_habari
Mkuu wa shirika rasmi la habari la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ameipongeza Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwa kupiga hatua za maendeleo katika nyuga mbalimbali ikiwemo sekta ya uandishi wa habari, huku akitoa mwito wa kuimarishwa ushirikiano wa pande mbili katika uga huo.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Nov 13, 2018 11:06 UTC
  • Kongo na Iran kuimarisha ushirikiano wao katika uga wa habari

Mkuu wa shirika rasmi la habari la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ameipongeza Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwa kupiga hatua za maendeleo katika nyuga mbalimbali ikiwemo sekta ya uandishi wa habari, huku akitoa mwito wa kuimarishwa ushirikiano wa pande mbili katika uga huo.

Lambert Kaboyi Abimana ameyasema hayo katika mazungumzo yake na Balozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran mjini Kinshasa, Jahanbakh Hassanzade na kuongeza kuwa, vyombo vya habari vina umuhimu mkubwa katika maendeleo na ustawi wa nchi yoyote ile.

Abimana ameliomba Shirika la Habari la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran IRNA kuandaa warsha za mara kwa mara zitakazowafaidi waandishi wa habari wa DRC.

Mkuu wa Shirika la Habari la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ameashiria kutiwa saini makubaliano ya kuimarisha ushirikiano kati ya Congo Press Agency na IRNA na kuishukuru Iran kwa kutangaza utayarifu wake wa kuwapokea wanachuo Wakongomani wanaotaka kuja hapa nchini kusomea shahada za uzamifu kwenye taaluma ya uandishi habari. 

Bendera za Iran na Kongo

Pande mbili hizo zimesisitizia umuhimu wa kufikishiwa habari sahihi wananchi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Kongo DR.

Shirika rasmi la habari la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na Shirika la Habari la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran IRNA yalitiliana saini ya kuimarisha ushirikiano wa pande mbili mwezi Novemba mwaka jana hapa mjini Tehran.