Waislamu Nigeria waandamana kulaani mauaji yaliyofanywa na jeshi
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i49503-waislamu_nigeria_waandamana_kulaani_mauaji_yaliyofanywa_na_jeshi
Waislamu Nigeria wameandamana nje ya ofisi za Tume ya Haki za Binaadamu katika mji mkuu Abuja, kulaani mauaji yaliyofanyika kati ya 27 hadi 30 Oktoba mwaka huu.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Nov 14, 2018 04:50 UTC
  • Waislamu Nigeria waandamana kulaani mauaji yaliyofanywa na jeshi

Waislamu Nigeria wameandamana nje ya ofisi za Tume ya Haki za Binaadamu katika mji mkuu Abuja, kulaani mauaji yaliyofanyika kati ya 27 hadi 30 Oktoba mwaka huu.

Akizungumza na Press TV mwanachama wa Harakati ya Kiislamu ya Nigeria Zuwairiyya Idris amesema wanajeshi wa Nigeria waliwaua shahidi karibu wafuasi 48 wa harakati hiyo katika matambezi ya amani ya Siku ya Arubaini ya mjukuu wa Mtume Muhammad SAW, Imam Hussein AS mjini Abuja. Amesema zaidi ya watu 100 walijeruhiwa huku wengine wakiwa mahututi. Taarifa zinasema idadi kubwa ya waliouawa au kujeruhiwa walikuwa chini ya umri wa miaka 18 huku wazazi waliouawa wakiachwa mayatima.

Bi. Idris aidha ameitaka serikali ya Nigeria imuachilie huru kiongozi wa Harakati ya Kiislamu ya Nigeria Sheikh Ibrahim Zakzaky. INM imetaka vikosi vya usalama vya Nigeria vitambue haki ya kuabudu ya wanachama wake.

Maandamano mjini Abuja ya kutaka Sheikh Zakzaky aachiliwe huru

Hali kadhalika amesisitiza kuwa wana haki ya kikatiba ya kushiriki katika maandamano ya amani na wametaka maafisa wa usalama waheshimu haki hiyo. Nasir Ladan wa Tume ya Haki za Binadamu Nigeria watachunguza malalamikio ya Harakati ya Kiislamu ya Nigeria na kutoa taarifa baada ya kukamilisha uchunguzi.

Katika tukio hilo la mwezi Oktoba la matambezi ya amani ya Siku ya Arubaini ya mjukuu wa Mtume Muhammad SAW, Imam Hussein AS mjini Abuja hivi karibuni wanajeshi wa Nigeria waliwahujumu washiriki na kuua shahidi Waislamu 48.