Watu wa nchi za Afrika wapinga vikali safari ya Mohammad bin Salman
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i49768-watu_wa_nchi_za_afrika_wapinga_vikali_safari_ya_mohammad_bin_salman
Watu wa nchi kadhaa za Afrika wamebainisha malalamiko yao makali kuhusu safari ya mrithi wa ufalme wa Saudi Arabia, Mohammad bin Salman katika nchi zao huku wakilaani vikali harakati zake za kushawishi nchi za Kiarabu ziwe na uhusiano wa kawaida na utawala wa Kizayuni wa Israel.
(last modified 2026-01-14T08:12:18+00:00 )
Nov 26, 2018 04:38 UTC
  • Watu wa nchi za Afrika wapinga vikali safari ya Mohammad bin Salman

Watu wa nchi kadhaa za Afrika wamebainisha malalamiko yao makali kuhusu safari ya mrithi wa ufalme wa Saudi Arabia, Mohammad bin Salman katika nchi zao huku wakilaani vikali harakati zake za kushawishi nchi za Kiarabu ziwe na uhusiano wa kawaida na utawala wa Kizayuni wa Israel.

Kwa mujibu wa televisheni ya Al Mayadeen malalamiko makali yameripotiwa katika nchi za Tunisia, Algeria, Misri na Mauritania ambazo Bin Salman anazitembelea. Wananchi wakiwemo shakhsia wa kisiasa na kiutamaduni katika nchi hizo wameandamana wakipinga safari ya Bin Salman huku wakitaka ifutwe. 

Jumuiya ya Waandishi Habari Tunisia imemuandikia barua Rais Beji Caid Essebsi na kuashiria jinai za kivita na dhidi ya binadamu za utawala wa Saudia na kusema safari ya Bin Salman inalenga kusafisha mikono yake iliyojaa damu. Aidha katika barua yao wamesema Bin Salman amehusika katika mauaji ya kuogofya ya mwandishi habari mkosoaji wa Saudia Jamal Khashoggi mjini Istanbul.

Barua hiyo imeongeza kuwa Bin Salman ni hatari kwa usalama na amani na kwamba mtawala huyo wa Saudia ni adui wa uhuru wa kujieleza.

Bin Salman analaumiwa kwa kumwaga damu za watu wasio na hatia

Mohammad Ali Ghadiri, Naibu mkuu wa Jumuiya ya Wafanyakazi Tunisia amesema kadhia ya Palestina ni kadhia muhimu zaidi kwa watu wa Tunisia na amesisitiza kuwa jinai hatua yoyote ya kuwa na uhusiano wa kawaida na utawala wa Kizayuni.

Naye Jamal bin Abdul Salam wa Chama cha Mrengo wa Algeria Mpya, amesema kuna hitilafu kubwa za kimtazamo baina ya Algeria na Saudia  kuhusu kadhia ya Palestina, vita dhidi ya Yemen na uhusiano na Iran. Amebainisha upinzani wake mkali kwa safari tarajiwa ya Bin Salman nchini humo.

Kwa upande wake Mohammad Oul Fal,  Mkuu wa Chama cha Al Refa cha Mauritania amepinga safari ya Bin Salman nchini humo na kusema Wamauritani wanapinga uhusiano na msimano wowote na utawala wa Saudia kutokana na jinai ambazo zimetendwa na utawala huo.