Askari wa China watumwa Sudan kulinda amani
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i50100-askari_wa_china_watumwa_sudan_kulinda_amani
Askari 100 wa kulinda amani wa China wameondoka Jumanne ya leo Beijing kuelekea Darfur, nchini Sudan kwa ajili ya majukumu ya kulinda amani kwa kipindi cha mwaka mmoja katika kikosi cha Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika (UNAMID).
(last modified 2026-02-21T22:51:18+00:00 )
Dec 11, 2018 12:04 UTC
  • Askari wa China watumwa Sudan kulinda amani

Askari 100 wa kulinda amani wa China wameondoka Jumanne ya leo Beijing kuelekea Darfur, nchini Sudan kwa ajili ya majukumu ya kulinda amani kwa kipindi cha mwaka mmoja katika kikosi cha Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika (UNAMID).

Askari hao ni kikundi cha kwanza cha timu ya askari 225 na ni kikosi cha 15 cha China kwenda mkoani Darfur; kikundi cha pili kinatarajiwa kuondoka China Disemba 18.

Kikosi hicho kitakuwa na jukumu la kusimamia mahitaji na miradi ya ukandarasi, kukarabati majengo, na kukarabati pamoja na kujenga nyumba, barabara, na viwanja vya ndege.

Askari wa China katika kikosi cha UNMID Sudan akitunukiwa nishani

Mwezi Julai mwaka huu, askari 140 wa kikosi cha helikopta cha kulinda amani cha China walitunukiwa "nishani ya amani" huko Darfur, Sudan.

Akizungumza kwenye hafla ya kuwatunuku nishani, mwakilishi UNAMID Jeremiah Mambolo alisema kikosi cha kulinda amani cha China tawi la helikopta, kimefanya kazi nzuri katika kuimarisha amani na ukarabati pamoja na kutoa msaada wa kibinadamu katika eneo la Darfur.

Kikosi cha pamoja cha AU na UN huko Darfur, nchini Sudan UNAMID kina askari 20,000 kutoka nchi 30 duniani ambapo kikosi hicho mwaka jana kiliongozewa muda mwingine wa mwaka mmoja wa kuhudumu nchini Sudan hadi mwisho wa mwezi wa Juni wa  2019.