Maandamano makubwa ya kupinga Uzayuni yafanyika nchini Nigeria
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i50230-maandamano_makubwa_ya_kupinga_uzayuni_yafanyika_nchini_nigeria
Maelfu ya wananchi wa Nigeria wamefanya maandamano dhidi ya Uzayuni kusini magharibi mwa nchi hiyo na kutangaza himaya na uungaji mkono wao kwa taifa madhulumu la Palestina.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Dec 17, 2018 11:46 UTC
  • Maandamano makubwa ya kupinga Uzayuni yafanyika nchini Nigeria

Maelfu ya wananchi wa Nigeria wamefanya maandamano dhidi ya Uzayuni kusini magharibi mwa nchi hiyo na kutangaza himaya na uungaji mkono wao kwa taifa madhulumu la Palestina.

Maandamano hayo yaliyofanyika katika mji wa Osun wa kusini magharibi mwa Nigeria yalishuhudia waandamanaji wakiwa wamebeba mabango na maberamu yenye maandishi mbalimbali ya kulaani jinai za utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya wananchi wa Palestina.

Aidha waandamanaji hao walisikika wakipiga nara za kuupinga Uzayuni pamoja na jinai zake huko Palestina inayokaliwa kwa mabavu.

Taarifa zaidi zinasema kuwa, Waandamani hao wamesisitiza juu ya kuundwa nchi huru ya Palestina mji mkuu wake ukiwa Beitul-Muqaddas. Katika upande mwingine, waandamanaji hao wameutaka Umoja wa Mataifa kuitambua nchi huru ya Palestina mji mkuu wake ukiwa Beitul-Muqaddas.

Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya akiwekeana saini mkataba na Benjami Netanyahu, Waziri Mkuu wa utawala dhalimu wa Israel

Hayo yanajiri katika hali ambayo, utawala haramu wa Israel unaotenda jinai kila uchao dhidi ya Wapalestina, katika miaka ya hivi karibuni umekuwa ukifanya juhudi za kujikurubisha zaidi kwa mataifa mbalimbali ya Kiafrika lengo likiwa ni kutekeleza mipango yake ya Kizayunii katika bara hilo.

Aidha kumekuwa kukitolewa tahadhari mbalimbali kuhusiana na njama za Israel za kutaka kujipenyeza zaidi barani Afrika. Baadhi ya ripoti zinaonyesha kuwa, idadi ya wafuasi wa utawala wa Kizayuni inaongezeka barani Afrika kutokana na nchi za Kiislamu na Kiarabu kushindwa kutekeleza wajibu wao barani humo. Pamoja na hayo, njama hizo zimekuwa zikikabiliwa na upinzani na maandamano katika nchi mbalimbali barani Afrika.