AU yatahadharisha kuhusu machafuko ya Libya
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i50281-au_yatahadharisha_kuhusu_machafuko_ya_libya
Mratibu wa Masuala ya Amani na Usalama wa Umoja wa Afrika amesema kuwa machafuko na ukosefu wa usalama nchini Libya vinaathiri bara zima la Afrika.
(last modified 2023-11-27T12:14:11+00:00 )
Dec 19, 2018 15:11 UTC
  • AU yatahadharisha kuhusu machafuko ya Libya

Mratibu wa Masuala ya Amani na Usalama wa Umoja wa Afrika amesema kuwa machafuko na ukosefu wa usalama nchini Libya vinaathiri bara zima la Afrika.

 Ismail Sharqi ambaye alikuwa akihutubia katika kituo cha Utafiti wa Masuala ya Ugaidi nchini Algeria ameashiria mafanikio ya nchi za Afrika katika kupambana na ugaidi katika miaka ya hivi karibuni lakini amekiri kwamba, hadi sasa kuna changamoto kubwa ya janga hilo hususan katika maeneo ya Sahel Afrika na kwamba hatari ya machafuko na ukosefu wa amani inatishia bara zima la Afrika.

Afisa huyo wa Umoja wa Afrika amesema miongoni mwa sababu za machafuko ya sasa katika eneo la Sahel Afrika ni ukosefu wa amani nchini Libya na kwamba hali ya nchi hiyo sasa inashughulisha zaidi fikra za maafisa wa usalama wa Algeria.

 Ismail Sharqi amesema nchi za kigeni zilizosaidia harakati za kubadilisha mfumo wa kisiasa nchini Libya mwaka 2011 zinachangia katika machafuko yanayoshuhudiwa katika eneo hilo.

Mratibu wa Usalama wa Umoja wa Afrika ametoa wito wa kuwepo ushirikiano baina ya umoja huo na Umoja wa Mataifa kwa ajili ya kutafuta suluhisho la mgogoro wa Libya na kuitisha chaguzi za bunge na rais wa nchi hiyo.