Chama tawala Kongo DR chataka kuangaliwa upya matokeo ya uchaguzi
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i50778-chama_tawala_kongo_dr_chataka_kuangaliwa_upya_matokeo_ya_uchaguzi
Baada ya kushindwa katika matokeo ya awali ya uchaguzi wa rais, muungano wa chama tawala huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo umetangaza kwamba, unayo haki ya kutaka kuangaliwa upya matokeo hayo.
(last modified 2023-11-27T12:14:11+00:00 )
Jan 10, 2019 16:03 UTC
  • Chama tawala Kongo DR chataka kuangaliwa upya matokeo ya uchaguzi

Baada ya kushindwa katika matokeo ya awali ya uchaguzi wa rais, muungano wa chama tawala huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo umetangaza kwamba, unayo haki ya kutaka kuangaliwa upya matokeo hayo.

Muungano huo wa 'Common Front for Congo' ambao hadi sasa ndio wenye madaraka nchini humo umesema kuwa, umepata taarifa ya matokeo ya awali yaliyotangazwa na Tume ya Uchaguzi CENI, lakini unayo haki ya kutaka kuangaliwa upya matokeo hayo. 

Lambert Mende, Msemaji wa Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo amesema kwamba matokeo hayo ya muda yaliyotangazwa tunayaangalia kwa kina na yatafuatiliwa na muungano huo kwa njia za kisheria. Emmanuel Ramazani Shadary, ndiye mgombea anayeungwa mkono na muungano wa Common Front for Congo.

Emmanuel Ramazani Shadary, mgombea anayeungwa mkono na muungano wa Common Front for Congo

Wakati huo huo, mgombea wa upinzani aliyetangazwa kushika nafasi ya pili katika matokeo hayo ya awali, Martin Fayulu, ametangaza kutoyakubali matokeo hayo na kuitaka Tume ya Uchaguzi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kusimamia kwa haki zoezi hilo.

Fayulu ni mgombea ambaye anaungwa mkono na Kanisa Katoliki nchini humo na ambaye kwa mujibu wa kanisa hilo ndiye aliyeshinda uchaguzi huo.