SAUTI, Burundi: Tutahudhuria mkutano wa EAC na tutautumia mkutano huo kuishitaki Rwanda
Serikali ya Burundi imetangaza kwamba itahudhuria mkutano wa viongozi wakuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki utakaofanyika mwanzoni mwa mwezi ujao.
Hayo yamesemwa na Jean Claude Karerwa, Msemaji wa Rais Pierre Nkurunziza wa nchi hiyo na kubainisha kwamba, vyovyote iwavyo Bujumbura itashiriki mkutano huo na si muhimu nani atakayeiwakilisha Burundi.
Kadhalika Karerwa amesema kwamba serikali ya Burundi itatumia fursa hiyo kuomba kifanyike kikao cha dharura kitakachojadili mzozo uliopo kati yake na Rwanda. Burundi na Rwanda zimekuwa katika mzozo tangu kulipojiri jaribio la mapinduzi ya kijeshi dhidi ya Rais Nkurunziza hapo tarehe 13 Mei 2015.
Kwa maelezo zaidi tujiunge na mwandishi wetu wa jijini Bujumbura, Hamida Issa…………./