Nchi za Afrika kuanzisha mkakati wa kuendeleza ulinzi wa mtoto
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i51054-nchi_za_afrika_kuanzisha_mkakati_wa_kuendeleza_ulinzi_wa_mtoto
Maofisa wanaohusika na ulinzi wa mtoto kutoka nchi na maeneo 27 watakutana nchini Namibia kwa mara ya kwanza kujadili mikakati ya sasa na ya baadaye ya kuanzisha ulinzi wa mtoto kwa ajili ya ofisi ya kikanda ya Mashariki na Kusini mwa Afrika, ESAF.
(last modified 2026-01-14T08:12:18+00:00 )
Jan 22, 2019 23:17 UTC
  • Nchi za Afrika kuanzisha mkakati wa kuendeleza ulinzi wa mtoto

Maofisa wanaohusika na ulinzi wa mtoto kutoka nchi na maeneo 27 watakutana nchini Namibia kwa mara ya kwanza kujadili mikakati ya sasa na ya baadaye ya kuanzisha ulinzi wa mtoto kwa ajili ya ofisi ya kikanda ya Mashariki na Kusini mwa Afrika, ESAF.

Msimamizi wa ulinzi wa Mtoto wa Namibia Bi. Christine Aochamus amesema, mkutano huo unatarajiwa kufanyika tarehe 11 mwezi ujao wa Februari mjini Windhoek na lengo lake ni kuongeza ufahamu katika masuala ya ukiukwaji wa haki za watoto.

Amesema moja ya mkakati ni kuhakikisha Mtandao wa Ulinzi wa Mtoto kupitia ushirikiano na wadau na pia kutambua njia za kuhusisha zaidi vyombo vya habari, vyombo vya kisheria na washirika wengine katika nchi husika.

Moja ya stratejia za mtandao huo ni kuhakikisha kuwa kunakuwa na ushirikiano bora na vyombo vya habari, idara za usalama na washirika wengine katika nchi husika.

Watoto wa shule barani Afrika

Msimamizi wa ulinzi wa Mtoto wa Namibia Bi. Christine Aochamus  amesema nchi yake inatambua changamoto nyingi zilizoko katika kadhia ya kuwalinda watoto. Amesema katika miaka ya hivi karibuni barani Afrika kumeshuhudiwa ongezeko la kutelekezwa watoto jambo ambalo limeibua tatizo sugu la watoto wa mitaani.