UN: Wakimbizi elfu nne wameondolewa Libya
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i51342-un_wakimbizi_elfu_nne_wameondolewa_libya
Shirika la Kuhudumia Wakimbizi la Umoja wa Mataifa (UNHCR) limeripoti kuwa tangu mwanzoni mwaka mwaka jana wa 2018 hadi sasa zaidi ya wakimbizi 4000 wameondolewa huko Libya.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Feb 05, 2019 00:15 UTC
  • UN: Wakimbizi elfu nne wameondolewa Libya

Shirika la Kuhudumia Wakimbizi la Umoja wa Mataifa (UNHCR) limeripoti kuwa tangu mwanzoni mwaka mwaka jana wa 2018 hadi sasa zaidi ya wakimbizi 4000 wameondolewa huko Libya.

Shirika hilo la Umoja wa Mataifa lililo na jukumu la kuratibu shughuli za kimataifa kwa ajili ya kuwalinda na kutatua matatizo ya wakimbizi na wahajiri duniani kote limeripoti kuwa katika mwaka jana uliopita wakimbizi wa Libya elfu 34 na 505 walipatiwa huduma za tiba. Ripoti hiyo imeongeza kuwa katika kipindi hicho, familia elfu sita na 219 pia zilipatiwa misaada ya fedha na ya chakula. Wakati huo huo shirika la UNHCR limesema kuwa tayari limewasajili karibu watu elfu 56 na 643 wanaotafuta hifadhi huko Libya. 

Itakumbukwa kuwa Libya imekuwa ikitumika kama lango la kuvukia mamia ya maelfu ya wahajiri na wakimizi wanaojaribu kuelekea Ulaya wakikimbia hali ya mchafukoge na hali mbaya ya kiuchumi, kijamii na kisiasa katika eneo la mashariki ya Kati na kaskazini mwa Afrika ambayo ni natija ya uingiliaji wa nchi za Magharibi. Miezi ya karibuni nchi za Ulaya nazo zimeainisha hatua kali za kukabiliana na wahajiri tajwa. 

Adha na masaibu yanayowapata wahajiri wanaoelekea Ulaya