Apr 18, 2016 04:48 UTC
  • Mapigano ya polisi na raia yaua watu kadhaa Congo DR

Mapigano yaliyotokea baina ya polisi na raia wa kusini mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo yamesababisha mauaji ya watu kadhaa.

Habari zinasema kuwa, mapigano hayo yalitokea jana katika eneo la Cellule Kanyina kwenye mji wa Kolwezi baada ya raia wawili kuuliwa na watu waliokuwa na silaha.

Wakazi wa eneo hilo waliwazuia polisi kuchukua maiti za raia hao wawili waliouawa, suala lililozusha machafuko baina ya pande mbili.

Polisi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo inasema raia waliokuwa na hasira walishambulia kituo cha polisi cha Cellule Kanyina na kupora mali zilizokuwemo.

Maeneo ya mashariki na kusini mwa Congo DR yamekuwa yakishuhudia machafuko ya mara kwa mara na ghasia zinazosababishwa na mgogoro wa makundi ya waasi yanayoendesha shughuli zao katika maeneo hayo.

Tags