Aghalabu ya nchi za Afrika haziungi mkono ubaradhuli
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i54030-aghalabu_ya_nchi_za_afrika_haziungi_mkono_ubaradhuli
Shirika la kutetea haki za binadamu la Human Rights Watch limesema zaidi ya nusu ya nchi za eneo la chini ya Jangwa la Sahara barani Afrika haziungi mkono ubaradhuli na uhusiano wa watu wa jinsia moja.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jun 10, 2019 03:24 UTC
  • Aghalabu ya nchi za Afrika haziungi mkono ubaradhuli

Shirika la kutetea haki za binadamu la Human Rights Watch limesema zaidi ya nusu ya nchi za eneo la chini ya Jangwa la Sahara barani Afrika haziungi mkono ubaradhuli na uhusiano wa watu wa jinsia moja.

Neela Ghoshal, mtaalamu wa HRW katika masuala ya ubaradhuli, ushoga, usagaji na watu waliobadilisha jinsia zao amesema nchi 28 kati ya 49 zilizoko chini ya Jangwa la Sahara zimepasisha sheria zinazopiga marufuku na kuharamisha uozo huo wa kijamii.

Amesema hukumu ya kunyongwa watu wanaojihusisha na uchafu huo imekuwa ikitekelezwa kwa mujibu wa Sharia za Kiislamu katika nchi za Mauritania, Sudan na baadhi ya maeneo ya Nigeria. 

Kwa mujibu wa mtaalamu huyo wa Human Rights Watch, wanaume wanaojihusisha na ushoga wamekuwa wakinyongwa pia huko kusini mwa Somalia, hususan katika maeneo yanayodhibitiwa na kundi la kigaidi la al-Shabaab.

Baadhi ya nchi za Magharibi pia zinapinga ushoga 

HRW imesema Chad, Nigeria na Burundi ima zimetunga sheria mpya za kupambana na ubaradhuli au zimeshadidisha adhabu katika sheria zilizokuwepo.

Mwezi uliopita, Mahakama Kuu ya Kenya ilitupilia mbali ombi la kutaka kubatilisha sheria zinazopiga marufuku uhusiano wa kimapenzi wa watu wa jinsia moja nchini humo.

Ni nchi tatu tu za Afrika za Angola, Msumbiji na Ushelisheli ambazo katika miaka ya hivi karibuni zimebatilisha au kuelegeza sheria za kupambana na ushoga na usagaji.