Chama cha FDU-Inkingi cha Rwanda: Kuuawa kwa visu kiongozi wetu hakutotunyamazisha
Chama cha upinzani cha FDU-Inkingi cha nchini Rwanda kimesema kuwa, kupigwa visu hadi kufa afisa mwandamizi wa chama hicho, hakutowanyamazisha na wataendelea na kampeni yao ya kuikosoa serikali ya Rais Paul Kagame.
Sylidio Dusabumuremyi, mratibu taifa wa chama cha upinzani FDU-Inkingi party, amepigwa visu hadi kufa katika eneo lake la kazi Jumatatu jioni.
Mkuu wa chama hicho Victoire Ingabire amethibitisha habari hiyo na kusema jana kwamba kushambuliwa na kuuliwa kwa kupigwa visu kunafanyika kwa ni ya kuwanyamazisha.
Kwa upande wao, maafisa wa serikali ya Rwanda wamesema kuwa, wameanzisha uchunguzi kuhusu shambulio hilo na tayari watu wawili wameshatiwa mbaroni kwa ajili ya kusailiwa.
Ingabire ameliambia shirika la habari la Reuters kwamba shambulio hilo limefanyika kwa nia ya kuwanyamazisha wapinzani. Wanajaribu kutuzuia kuunda chama cha upinzani.
Mkuu huyo wa chama cha FDU-Inkingi mwenyewe anakabiliwa na mashtaka kadhaa ya ugaidi. Alisema jana Jumanne wakati akifika mahakamani kusikilia kesi zinazohusiana na ugaidi zinazomkabili yeye na wenzake tisa, kwamba kunafanyika mauaji na mashambulizi dhidi ya viongozi wa chama chake ili kuwaziba midomo.
Itakumbukuwa kuwa, mwaka 2010, Victoire Ingabire alifungwa jela nchini Rwanda kwa kuwataka maafisa wa nchi hiyo wakitambue rasmi chama chake.

Afisa aliyeuawa kwa kupigwa visu alikuwa takriban ni msaidizi wa pili wa Ingabire kuuawa mwaka huu. Msemaji wa Ingabire naye alipatikana ameuawa mwezi Machi mwaka huu.
Victoire Ingabire alirejea nchini Rwanda mwaka 2010 baada ya kukaa uhamishoni nchini Uholanzi kwa muda wa miaka 16.
Taarifa zinasema kuwa, Dusabumuremyi ni kiongozi wa sita wa chama cha upinzani cha FDU kuuawa nchini Rwanda katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita.