Mamia waandamana Guinea Conakry dhidi ya Rais wa nchi hiyo
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i56833-mamia_waandamana_guinea_conakry_dhidi_ya_rais_wa_nchi_hiyo
Maelfu ya wananchi wa Guinea Conakry wamefanya maandamano katika mji mkuu wa nchi hiyo katika fremu ya upinzani dhidi ya mpango wa rais Alpha Conde wa nchi hiyo wa kutaka kugombea nafasi hiyo kwa mara ya tatu mfululizo.
(last modified 2026-01-14T08:12:18+00:00 )
Oct 24, 2019 23:20 UTC
  • Mamia waandamana Guinea Conakry dhidi ya Rais wa nchi hiyo

Maelfu ya wananchi wa Guinea Conakry wamefanya maandamano katika mji mkuu wa nchi hiyo katika fremu ya upinzani dhidi ya mpango wa rais Alpha Conde wa nchi hiyo wa kutaka kugombea nafasi hiyo kwa mara ya tatu mfululizo.

Waandamanaji hao waliokuwa wakipiga nara zinazosema "Haiwezekani", wameitaka serikali ya Conakry kuwaachia huru wafungwa wa kisiasa.

Maandamano hayo yameitishwa na muungano wa National Front for the Defence of the Constitution (FNDC) wa wanasiasa wanaopinga jaribio la Rais Conde la kubadilisha katiba ya nchi na kumruhusu kugombea nafasi hiyo kwa mara ya tatu mfululizo.

Maandamano mengine kama hayo yameshuhudiwa pia katika miji mingine ya Guinea Conakry chini ya ulinzi mkali wa polisi.

Guinea Conakry

Jumanne iliyopita viongozi 12 wa kundi la FNDC walihukumiwa vifungo vya hadi mwaka mmoja jela kwa kuitisha maandamano ya wiki iliyopita ya wananchi. Katika maandamano hayo polisi ya Guinea iliwapiga risasi waandamanaji na kuua 9 miongoni mwao.

Rais Alpha Conde wa Guinea (81) ambaye kipindi chake cha pili cha urais kinamalizika mwakani, ameitaka serikali ichunguze uwezekano wa kubadilisha katiba na kumruhusu kugombea tena kiti cha rais katika uchaguzi ujao.