Abiy Ahmed: Watu 86 wameuawa katika machafuko ya karibuni Ethiopia
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i57064-abiy_ahmed_watu_86_wameuawa_katika_machafuko_ya_karibuni_ethiopia
Waziri Mkuu wa Ethiopia amesema kuwa, watu 86 wameuawa katika maandamano ya kupinga serikali yaliyotokea mwezi uliopita nchini humo.
(last modified 2026-01-14T08:12:18+00:00 )
Nov 04, 2019 23:22 UTC
  • Abiy Ahmed: Watu 86 wameuawa katika machafuko ya karibuni Ethiopia

Waziri Mkuu wa Ethiopia amesema kuwa, watu 86 wameuawa katika maandamano ya kupinga serikali yaliyotokea mwezi uliopita nchini humo.

Shirika la habari la Reuters limemnukuu Abiy Ahmed akisema hayo jana na kuongeza kuwa, idadi ya watu waliouawa katika machafuko ya mwezi uliopita wa Agosti 2019 imeongezeka na kufikia 86.

Amefafanua zaidi kwa kusema, idadi ya awali iliyotangazwa na serikali ilikuwa watu 78 hata hivyo idadi hiyo imeongezeka na kufikia watu 86, 82 kadi yao ni wanaume na wanne ni wanawake.

Kabla ya hapo, Waziri Mkuu huyo wa Ethiopia alikuwa ametangaza kuwa, wengi wa waliouawa ni watu wa makabila ya Oromo na Amhara na ni Waislamu kwa Wakristo.

Machafuko ya mwezi Oktoba 2019 yalitokea katika miji kadhaa ya eneo la Oromiya lenye idadi kubwa zaidi ya watu nchini Ethiopia.

Umoja wa Mataifa umesema kuwa, machafuko hayo yameshapelekea zaidi ya watu milioni mbili kuwa wakimbizi.