Sudan na Chad zapokea makumi ya wahajiri waliotimuliwa Libya
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i57346-sudan_na_chad_zapokea_makumi_ya_wahajiri_waliotimuliwa_libya
Serikali ya Libya imewahamishia katika nchi za Sudan na Chad makumi ya wahamiaji haramu.
(last modified 2023-11-27T12:14:11+00:00 )
Nov 18, 2019 11:38 UTC
  • Sudan na Chad zapokea makumi ya wahajiri waliotimuliwa Libya

Serikali ya Libya imewahamishia katika nchi za Sudan na Chad makumi ya wahamiaji haramu.

Katika taarifa, Idara ya Kusimamia Uhamiaji katika mji wa mashariki wa Benghazi nchini Libya imeripoti kuwa, wahajamiaji haramu 65 wamepelekwa katika nchi za Sudan na Chad kupitia mpaka wa kusini.  

Mwezi uliopita, idara hiyo iliripoti kuwa, wahamiaji haramu wengine 95 wamepelekwa nchini Misri kwa kutumia usafiri wa mabasi.

Siku chache kabla ya hapo pia, idara hiyo ya kusimamia masuala ya wahajiri iliwahamishia katika nchi za Nigeria na Misri wahamiaji haramu wengine zaidi ya 100. 

Wahamiaji haramu nchini Libya

Kwa mujibu wa Shirika la Kuhudumia Wakimbizi la Umoja wa Mataifa (UNHCR), Rwanda imewapokea wakimbizi 189 kutoka Libya kufikia sasa. Serikali ya Kigali imesema iko tayari kuwapokea na kuwapa hifadhi wakimbizi 30,000 kutoka Libya lakini itawakaribisha kwa utaratibu maalumu na katika hatua kadhaa.

Shirika la Kimataifa la Uhamiaji (IOM) limeripoti kuwa, kuna wakimbizi na wahamiaji haramu 650,000 nchini Libya, ambapo 6,000 miongoni mwao, wakiwemo wanawake na watoto wadogo wanazuiliwa katika vituo mbalimbali.