Wakenya wanaoishi nje ya nchi watuma nyumbani dola bilioni 2.546
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i58028-wakenya_wanaoishi_nje_ya_nchi_watuma_nyumbani_dola_bilioni_2.546
Raia wa Kenya wanaoishi na kufanya kazi nje ya nchi hiyo wametuma nyumbani dola bilioni 2.546 za Kimarekani sawa na Ksh. bilioni 256.4 katika kipindi cha miezi 11 ya mwaka 2019 ikiwa ni ongezeko la asilimia 3.8 ikilinganishwa na kipindi sawa na hicho mwaka jana.
(last modified 2026-03-27T07:58:19+00:00 )
Dec 21, 2019 21:45 UTC
  • Wakenya wanaoishi nje ya nchi watuma nyumbani dola bilioni 2.546

Raia wa Kenya wanaoishi na kufanya kazi nje ya nchi hiyo wametuma nyumbani dola bilioni 2.546 za Kimarekani sawa na Ksh. bilioni 256.4 katika kipindi cha miezi 11 ya mwaka 2019 ikiwa ni ongezeko la asilimia 3.8 ikilinganishwa na kipindi sawa na hicho mwaka jana.

Kwa ujumla mwaka jana, kiwango cha fedha zilizotumwa na Wakenya wanaofanya kazi nje ya nchi kiliongezeka kwa asilimia 40.7  ikilinganishwa na mwaka 2017.

Amerika ya Kaskazini inaongoza kwa kiwango cha pesa zinazotumwa ambazo ni asilimia 47.84  huku walio katika nchi za Ulaya wakituma asilimia 23.9 na Wakenya katika maeneo mengine duniani wakichangia asilimia 28.07.

Fedha zinazotumwa na Wakenya walio nje ya nchi ndio chanzo kikubwa zaidi cha fedha za kigeni kwa nchi hiyo katika hali ambayo miaka ya nyuma chanzo kikubwa cha pato la fedha za kigeni Kenya kilikuwa ni utalii, mauzo ya chai, maua na matunda.

Kuimarika njia za kutuma fedha kumepelekea idadi kubwa ya Wakenya waweze kutuma pesa nyumbani

Kutumwa fedha hizo za kigeni, ambazo aghalabu huwa ni dola ya Marekani ni jambo ambalo limepelekea shilingi ya Kenya kuimarika mkabala wa sarafu za kigeni.

Gavana wa Benki Kuu ya Kenya Patrick Njoroge amesema kuimarika njia za kutuma fedha ndio sababu ya ongezeko la fedha zinazotumwa nchini na Wakenya wanaoishi ughaibuni.

Weledi wa mambo wanasema kiwango cha pesa zinazotumwa na Wakenya walioko nje ya nchi ni zaidi ya hicho kilichotajwa kwa kuzingatia kuwa wengine hutuma fedha zao kwa njia zisizo rasmi.