Watu 17 wauawa katika shambulizi la kuvizia mashariki mwa Congo DR
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i60589-watu_17_wauawa_katika_shambulizi_la_kuvizia_mashariki_mwa_congo_dr
Watu wasiopungua 17 wameuawa na wengine kadhaa kijeruhiwa katika shambulizi lililolenga gari lililokuwa na walinzi wa mbuga ya taifa na abiria kadhaa huko mahariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
(last modified 2026-02-21T22:51:18+00:00 )
Apr 25, 2020 02:57 UTC
  • Watu 17 wauawa katika shambulizi la kuvizia mashariki mwa Congo DR

Watu wasiopungua 17 wameuawa na wengine kadhaa kijeruhiwa katika shambulizi lililolenga gari lililokuwa na walinzi wa mbuga ya taifa na abiria kadhaa huko mahariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Ripoti zinasema kuwa, walinzi 12 wa Mbuga ya Taifa ya Virunga huko mashariki mwa Congo DR, dereva wao na raia wengine 4 wameuawa katika shambulizi hilo lililofanywa na wanamgambo wenye silaha. Raia wengine wanne wamejeruhiwa.

Yunus Pandasi ambaye ni miongoni mwa viongozi wa taasisi za kiraia nchini Congo amesema kuwa mauaji hayo yamefanywa na wanamgambo wa Kihutu kutoka Rwanda. 

Waasi wa Kihutu, Congo DR

Mbuga ya Taifa ya Virunga iko katika mpaka wa nchi tatu za Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Uganda na Rwanda na imepata umashuhuri wa kimataifa kutokana na kuwa na Sokwe Watu wanaopatikana kwa wingi zaidi katika eneo hilo la dunia. 

Eneo la mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo limekuwa likishuhudia machafuko ya mara kwa mara baina ya makundi ya wanamgambo kutokana na kuwa na utajiri kubwa wa madini hususan dhahabu na almasi.