de Souza: Sera ya Marekani kuhusu Afrika ni kupunguza jamii ya Waafrika
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i60621-de_souza_sera_ya_marekani_kuhusu_afrika_ni_kupunguza_jamii_ya_waafrika
Mtaalamu wa masuala ya jamii wa Marekani amefichua kuwa, siasa za nje za serikali mbalimbali za Marekani kuhusuana na Afrika zinalenga kupunguza jamii ya watu wa bara hilo.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Apr 26, 2020 20:11 UTC
  • de Souza: Sera ya Marekani kuhusu Afrika ni kupunguza jamii ya Waafrika

Mtaalamu wa masuala ya jamii wa Marekani amefichua kuwa, siasa za nje za serikali mbalimbali za Marekani kuhusuana na Afrika zinalenga kupunguza jamii ya watu wa bara hilo.

Raymond de Souza ambye ni Mkuu wa Taasisi ya Sacred Heart mjini New York amefichua kuwa, siasa za serikali ya sasa ya Marekani ni zilezile za katikati ya muongo wa 1970 wakati Henry Kissinger alipokuwa waziri wa mambo ya nje wa Marekani na zingali zinaendelezwa hadi hii leo. 

de Souza amesema kuwa lengo la siasa za nje za Marekani barani Afrika ni kupunguza jamii ya Waafrika, kwa msingi huo misaada ya Washington kwa nchi za bara la Afrika haitolewi katika kalibu ya kuwawezesha watu kupata maji safi au huduma za elimu na kadhalika, bali zaidi kwa shabaha ya kusaidia kutoa na kuzuia mimba ili kupunguza jamii ya Waafrika.

Mtaalamu huyo wa masuala ya kijamii ameongeza kuwa, Afrika ina maliasili na rasilimali nyingi, na wakati wa Henry Kissinger na baada yake Marekani imekuwa ikifanya mikakati ya kuhakikisha kwamba, Afrika haipigi hatua muhimu za maendeleo wala Waafrika hawafaidiki na maliasili na rasilimali hizo kwa sababu Marekani inazihitajia. 

Afrika

Msomi huyo ameashiria ushirikiano wa nchi za Magharibi katika siasa na sera hizo za kulibakisha nyuma bara la Afrika kwa maslahi yao na kusema: Mwaka 1990 hadi 2000 Marekani, Canada na Ulaya zilitenga karibu dola bilioni sita kwa ajili ya programu ya kudhamini fivaa vya kuzuia na kuavya mimba barani Afrika badala ya kutenga fedha hizo kwa ajili ya kudhamini maji safi ya kunwa, chakula au mapambano dhidi ya ugonjwa wa malaria unaoangamiza maelfu ya watu katika nchi za Afrika. 

 Raymond de Souza amesisitiza kuwa, lengo kuu ni kuwaacha Waafrika waangamie.